1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Limassol, Cyprus. Ujerumani atembelea majeshi ya Ujerumani, Cyprus.

4 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCw8

Waziri wa ulinzi wa Ujerumani Franz Joseph Jung yuko katika mji wa bandari wa Limassol nchini Cyprus kuyatembelea majeshi ya Ujerumani yanayotumika katika jeshi la umoja wa mataifa la kulinda amani nchini Lebanon , UNIFIL.

Kufuatia mazungumzo mjini Beirut na Tel Aviv , Jung amesema anataka kupata habari zaidi juu ya ujumbe wa jeshi la majini unaoongozwa na Ujerumani, ambao una lengo la kuzuwia kuingizwa kwa silaha kinyume na sheria kwa jeshi la wanamgambo wa Hizboullah ikiwa ni kwa mujibu wa makubaliano ya kusitisha mapigano na Israel.

Hapo mapema Jung amesema Israel imemhakikishia kuwa hakutakuwa na marudio ya tukio ambapo ndege za kijeshi za Isreal ziliruka chini chini na kufyatua makombora karibu na meli ya kivita ya Ujerumani.

Wakati huo huo , waziri mkuu wa Lebanon Fouad Siniora ameondoa marufuku ya kutokuwa na chombo chochote cha kijeshji katika eneo la maili sita katika mwambao wa pwani ya nchi hiyo ili kutoa nafasi kwa jeshi la majini la Ujerumani kufanya doria kwa nafasi zaidi.