1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LISBON: Kipaumbele ni mgogoro wa Mashariki ya Kati

19 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBhA

Viongozi wa kundi la nchi nne kuhusu Mashariki ya Kati,hii leo wanakutana pamoja na waziri mkuu wa zamani wa Uingereza,Tony Blair katika mji wa Lisbon nchini Ureno.

Blair,aliechaguliwa hivi karibuni kama mjumbe maalum wa kundi hilo kutafuta suluhisho la amani kwa mgogoro wa Mashariki ya Kati,anatazamiwa kutoa mpango utakaoweka msingi wa kuundwa taifa la Palestina katika siku zijazo.

Majadiliano ya viongozi hao vile vile yanatazamiwa kutoa kipaumbele kwa wito uliotolewa na Rais George W.Bush wa Marekani hivi karibuni kuwa mchakato wa amani unahitaji kupigwa jeki.