1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LISBON:Mkutano wa viongozi wa Umoja wa Ulaya umeanza

18 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Ei

Viongozi wa nchi na serikali za Umoja wa Ulaya leo wameanza mkutano wa siku mbili mjini Lisbon, Ureno kujadili makubaliano ya kutiwa saini mkataba mpya wa mageuzi.

Mkataba huo utachukuwa nafasi ya katiba ya Umoja wa Ulaya ya hapo awali iliyokataliwa na wananchi wa Ufaransa na Uholanzi katika kura ya maoni ya mwaka 2005.

Malalamiko yaliyowasilishwa na Poland na Italia ndio yanatazamiwa kuwa kikwazo katika mazungumzo hayo ya siku mbili.

Iwapo makubaliano yatafikiwa basi mageuzi hayo mapya huenda yakaanza kutumika mwanzo mwa mwaka 2009 kabla ya uchaguzi ujao wa Umoja wa Ulaya.