1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON : Ajali ya helikopta yauwa sita

28 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCfh

Takriban watu sita wameuwawa katika ajali ya kuanguka kwa helikopta nje ya mwambao wa kaskazini magharibi wa Uingereza.

Helikopta hiyo ya kiraia ilikuwa imebeba wafanyakazi wake wawili na waajiriwa watano wa kampuni ya nishati ya Centrica wakati ilipoanguka.Waokowaji wanasema maiti sita zimepatikana kwenye bahari ya Ghuba ya Morecambe na mtu mwengine mmoja bado hajulikani alipo.

Polisi inasema kwamba inaendelea kumtafuta mtu huyo wa saba.