1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

London. Angela na Tony wakubaliana kushirikiana.

4 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCw9

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair wamekubaliana kuwa suala la mapambano dhidi ya hali ya ujoto duniani liwe katika ajenda ya juu kimataifa.

Kufuatia mkutano wao mjini London, kansela Merkel amewaambia waandishi wa habari kuwa mabadiliko ya hali ya hewa ni changamoto kubwa katika karne hii ya 21.

Waziri mkuu Tony Blair ameahidi kuiunga mkono Ujerumani katika juhudi zake wakati itakapochukua urais wa kundi la mataifa yenye viwanda G8 pamoja na urais wa umoja wa Ulaya.