1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON: Batamzinga wenye homa ya ndege waangamizwa, Uingereza.

4 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCV2

Maafisa wa afya nchini Uingereza wamewateketeza maelfu ya batamzinga kwenye shamba moja mashariki mwa nchi hiyo, ili kudhibiti maenezi ya homa hatari ya ndege.

Shughuli ya kuwaangamiza batamzinga hao kiasi laki moja na elfu sitini inatarajiwa kuendelea kwa muda wa siku mbili zijazo.

Karibu batamzinga elfu mbili na mia tano walikufa kwenye shamba lililoko katika eneo la Suffolk kutokana na homa hiyo.

Homa hiyo inayosababishwa na virusi aina ya H5N1 tayari imesababisha vifo vya watu zaidi ya mia moja na sitini kote duniani tangu miaka minne iliyopita.

Watu wengi waliofariki kwa sababu ya homa hiyo wanatoka barani Eshia.

Wataalamu wanachelea huenda virusi hivyo vikabadilika kwa hali ya kuweza kuambukiza binadamu kwa urahisi.

Maafisa wa afya wamesema hali imedhibitiwa na wakazi wa eneo hilo hawamo hatarini.