1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

London. Blair ang’atuka , na Brown mrithi wake.

11 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC3B

Waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair anatarajiwa kung’atuka kutoka madarakani ifikapo Juni 27. Blair amewaambia wafuasi wake kuwa licha ya utata mkubwa uliojitokeza kutokana na majeshi ya Iraq nchini Iraq, amekuwa wakati wote akifanya kile alichohisi kuwa ni sahihi kwa nchi yake.

Pongezi kwa Blair zimekuwa zikimiminika kutoka mataifa ya nje duniani kote, wakati rais wa Marekani George W. Bush akimsifu kuwa kama kiongozi wa kipekee.

Rais wa kamisheni ya Ulaya Jose Manuel Barosso amemsifu Blair kwa juhudi zake katika muda wa muongo mmoja uliopita kuiingiza Uingereza zaidi katika umoja wa Ulaya.

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema anasikitika kutokana na uamuzi huo wa Blair wa kujiuzulu , na kuongeza kuwa Blair amekuwa akiaminika sana katika masuala yote ya kimataifa na Ulaya.

Waziri wa fedha nchini Uingereza Gordon Brown anatarajiwa kuchukua nafasi ya Blair akiwa kiongozi wa chama cha Labour na waziri mkuu.