1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON: Blair asema Uingereza haitayumbishwa na Iran

2 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCD0

Waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair amesema kukiri kwa wanamaji wa Uingereza wanaozuiliwa na Iran kulikoonyeshwa kwenye runinga inayomilikiwa na serikali ya Iran, hakutabadili msimamo wake katika mzozo huo wa kidplomasia.

Vyombo vya habari vya Iran vimeripoti kwamba mabaharia wote 15 wamekiri walifanya makosa kwa kuingia eneo la bahari lililo himaya ya Iran katika ghuba la Uajemi bila kibali.

Mabaharia hao wanaendelea kuzuiliwa kwa wiki ya pili tangu walipokamatwa na Uingereza inajaribu kuwafikia.

Televisheni ya Iran imetangaza leo kwamba sera ya Uingereza imebadilika hatua ambayo huenda ikasaidia kuumaliza mzozo wa mabaharia 15 wanaozuiliwa na Iran.