1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON : Hakuna ukiukaji wa usalama wa kibiolojia

6 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBbc

Wakaguzi wa afya na usalama wameitembelea maabara moja ya utafiti kusini mwa Uingereza ambayo ilitajwa kuwa inaweza kuwa chanzo cha mripuko wa ugonjwa wa midomo na miguu kwa wanyama na maabara hiyo ya chanjo imesema leo hii haikugunduwa ushahidi wa ukiukaji wa taratibu za usalama wa kibilojia.

Wataalamu wa wanyama walikilinganisha kirusi kilichogunduliwa kwenye n’gombe katika shamba nje ya Wanborough maili 30 kusini magharibi mwa London na kile cha maabara ilioko karibu ambacho kilitumiwa kutengenezea chanjo dhidi ya ugonjwa huo.

Martin Shirley Mkurugenzi wa Afya ya Wanyama mjini London amesema ikiwa ni ziada ya ukaguzi mkubwa katika usalama wa kibiolojia,zana na taratibu, vikwazo vya kinga ya maambukizi na kadhalika ambavyo haukukonyesha ukiukaji wa taratibu zao wameweza kukaguwa rekodi hususan kwa ajili ya matumizi ya kirusi hicho.

Nchini Ujerumani mashamba matano yamefungwa kama hatua ya tahadhari kwa sababu yalikuwa na wanyama walioingizwa hivi karibuni kutoka kusini mwa Uingereza.