1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

London. Iran kuwekewa vikwazo.

7 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD58

Mataifa sita yenye nguvu duniani yanayojaribu kuishawishi Iran kusitisha urutubishaji wake wa madini ya Urani yamekubaliana kujadili uwezekano wa kuiwekea vikwazo nchi hiyo.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Uingereza Margaret Beckett ametangaza hayo baada ya kuwa mwenyeji wa mkutano huo mjini London pamoja na mawaziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani, Russia, China, Marekani na Ufaransa.

Hatua hiyo inakuja zaidi ya mwezi mmoja baada ya Iran kushindwa kutimiza masharti ya muda wa mwisho uliowekwa na baraza la usalama la umoja wa mataifa wa kusitisha shughuli hizo za urutubishaji madini ya Urani.

Baadhi ya mataifa ya magharibi yanahofu kuwa Iran inataka kutengeneza bomu la kinuklia . Iran inasisitiza wakati wote kuwa mpango wake wa kinuklia ni kwa ajili ya matumizi ya amani.