1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

London. Kimbunga chaharibu majengo na mali nyingine.

8 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CClY

Kimbunga kidogo lakini chenye nguvu kimelikumba eneo la maazi kaskazini magharibi ya mji wa London jana, na kuwajeruhi watu sita na kuharibu kiasi cha nyumba 100. Picha za televisheni zilionyesha uharibifu mkubwa katika eneo la Kensal Rise, ikiwa miti imeangushwa na magari kuharibiwa na vitu vinavyoanguka.