1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON: Mswada wa azimio kuimarisha vikwazo

3 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/C7AM

Maafisa kutoka nchi tano wanachama wa kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa pamoja na Ujerumani,wamekubaliana kutayarisha mswada wa azimio la tatu la Umoja wa Mataifa kuishinikiza Iran kuhusika na mradi wake wa nyuklia.Inatazamiwa kuwa Iran itawekewa vikwazo zaidi.

China na Urusi ambazo hapo awali hazikuwepo tayari kuunga mkono hatua kali kuchukuliwa dhidi ya Iran,safari hii zimeashiria kuregeza msimamo huo.Azimio jipya litapigiwa kura na Baraza la Usalama ikiwa ripoti za Umoja wa Ulaya na Shirika la Kimataifa la Nishati ya Nyuklia-IAEA zitasema, Iran haikufanya maendeleo ya kushirikiana na wakaguzi wa kimataifa.

Wanadiplomasia waliokutana siku ya Ijumaa mjini London,watakuwa na majadiliano mengine tarehe 19 Novemba kutathmini ripoti zinazongojewa.Iran inashikilia kuwa mradi wake wa nyuklia ni kwa ajili ya matumizi ya amani na inakanusha shutuma kuwa inalenga kutengeneza silaha za nyuklia.