1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON: Mwanamfalme Harry wa Uingereza hatopelekwa Iraq

17 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC1K

Wizara ya ulinzi ya Uingereza imethibitisha kuwa Mwanamfalme Harry hatopelekwa Iraq.Mkuu wa majeshi ya Uingereza,Jemadari Sir Richard Dannat amesema,jeshi limepata taarifa kuhusu idadi kadhaa ya vitisho maalum vilivyotolewa dhidi ya Harry pindi atapelekwa Iraq.Amesema,kwa sababu hiyo,ni hatari sana kwa mwanamfalme huyo na hata wanajeshi wenzake.Harry mwenye miaka 22 ni luteni wa pili katika kikosi kilichoanza kupelekwa mji wa Basra,kusini mwa Iraq.