1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON: Rice ataraji kukutana na Olmert na Abbas

19 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCZk

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Condoleezza Rice amesema anatumai kukutana na waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert na rais wa Wapalestina Mahmoud Abbas katika muda wa mwezi mmoja ujao.Azma ya mkutano huo ni kujaribu kufufua utaratibu wa amani wa Mashariki ya Kati.Rice alitamka hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari waliofuatana nae London ambako ameonana na waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair.Hapo kabla,Rice alikutana na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel mjini Berlin.