1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON: Terry Waite ajitolea kwenda Iran

31 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCDg

Mpatanishi wa Kingereza Terry Waite ambae binafsi aliwahi kuzuiliwa mateka,amejitolea kwenda Iran kujaribu kupata uhuru wa wanamaji 15 wa Kingereza waliozuiliwa nchini Iran.Waite alizuiliwa kwa miaka mitano nchini Lebanon baada ya kutekwa nyara na kundi la “Islamic Jihad” katika mwaka 1987.Kwa upande mwingine,ripoti zinasema, Uingereza imejibu barua iliyoandikwa na Iran kuhusika na kuzuiliwa kwa wanamaji 15 wa Kingereza.Waziri wa nje wa Uingereza Margaret Beckett,alipozungumza kando ya mkutano wa mawaziri wa nje wa Umoja wa Ulaya mjini Bremen,alisema,sasa pande mbili zinajadiliana.Wanamaji hao 15 wanatuhumiwa na Iran kuwa waliingia eneo la bahari la Iran,lakini Uingereza inasema walikuwa katika eneo la Irak.