1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

London. Uingereza kuanzisha sheria mpya dhidi ya ugaidi.

7 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBu7

Waziri wa mambo ya ndani wa Uingereza John Reid atatoa mapendekezo kadha ya sheria zenye utata dhidi ya ugaidi leo Alhamis, ikiwa ni pamoja na kurefusha kupita siku 28 muda ambao mtuhumiwa anaweza kuwekwa rumande bila ya kushtakiwa.

Mapendekezo hayo ambayo huenda pia yakaelekeza katika kuruhusu usikilizwaji wa simu za watu binafsi, hatua ambayo itatumika kama ushahidi mahakamani, yanaweza kuwa sehemu ya sheria ya hapo baadaye katika mapambano dhidi ya ugaidi, lakini inaelekea kuwa itazusha mjadala mkali bungeni.

Waziri mkuu anayeondoka madarakani Tony Blair ilibidi kuachana na juhudi za hapo kabla za kuongeza muda wa kuwekwa kizuizini hadi siku 90 baada ya baraza la wawakilishi kupinga hatua hiyo mwaka 2005. Ripoti za magazeti mwishoni mwa wiki zimesema kuwa mapendekezo hayo yanaungwa mkono na Gordon Brown, ambaye atachukua nafasi ya Blair kama waziri mkuu mwishoni mwa mwezi Juni.