1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

London. Uingereza kupunguza kesi za carbon kwa kuweka sheria maalum.

14 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCJO

Uingereza imekuwa nchi ya kwanza kutoa pendekezo la kisheria la kuweka viwango vya utoaji wa gesi zinazoharibu mazingira za Carbon Dioxide.

Sheria ya Mabadiliko ya hali ya hewa inaweka muda maalum wa kupunguza utoaji wa gesi hizo kwa asilimia 60 ifikapo mwaka 2050.

Waziri mkuu Tony Blair amesema mpango huo unaonyesha Uingereza inavyoongoza dunia katika kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa. Hii inakuja kiasi cha siku kadha tu baada ya viongozi wa umoja wa Ulaya kukubaliana katika mkutano mjini Brussels kupunguza gesi ya kaboni kwa asilimia 20 ifikapo mwaka 2020.