1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

London. Uingereza kutengeneza nyambizi za kisasa za kinuklia.

5 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCmG

Waziri mkuu Tony Blair amezindua mpango wa kuzifanyia mabadiliko ya kisasa silaha za kinuklia nchini Uingereza, kwa kupata nyambizi za kisasa za kinuklia.

Gharama ya nyambizi hizo mpya, ambazo zitabeba makombora ya kinuklia , itakuwa kati ya Euro bilioni 22 na 30. Waziri mkuu wa Uingereza ameliambia bunge kuwa kuna kitisho kipya kutoka katika mataifa kama Korea ya kaskazini na Iran. Blair pia amehidi kupunguza hazina ya mabomu ya kinuklia kwa asilimia 20 kutoka kiasi cha mabomu 200 ya hivi sasa hadi 160.