1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON : Uingereza yachunguza kifo cha Latvinenko

25 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCpR

Polisi ya Uingereza leo imekuwa mbioni kutaka kujuwa vipi mpelelezi wa zamani wa Urusi Alexander Litvinenko ametiwa sumu ya miale ya nuklea na nani anayehusika na kifo chake.

Magazeti ya Uingereza yamemuanika Rais Vladimir Putin wa Urusi kuhusika na kifo hicho baada ya Litvinenko kuushutumu utawala wa Urusi kwa kumuuwa katika ujumbe alioutowa wakati akiwa mahtuti kitandani na hiyo kutishia suala hilo kupamba moto kisiasa.

Kiwango kikubwa cha sumu ya miale ya nuklea kutoka madini ya plutonium kimeonekana kwenye mkojo wa Litvinenko wakati uchunguzi pia umefanyika kwa watu waliokuwa na mawasiliano na kachero huyo wa zamani wa Urusi.

Litvinenko mpizani wa serikali ya Urusi amehamia nchini Uingereza miaka sita iliopita na amechukuwa uraia wa nchi hiyo na wakati wa kifo chake alikuwa akichunguza kuuwawa kwa kupigwa risasi mjini Moscow mwezi uliopita kwa mwandishi wa habari wa kike wa Urusi Anna Politkovskaya ambaye alikuwa pia mpizani wa Putin.

Ikulu ya Russia imekanusha kuhusika na kifo hicho.