1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON: Uingereza yapunguza kitisho dhidi ya usalama wa kitaifa

5 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBlk

Waziri wa maswala ya ndani wa Uingereza, Jacqui Smith, ametangaza kwamba kiwango cha kitisho kwa usalama wa taifa kimepungua kutoka kilipokuwa wiki iliyopita baada ya njama ya mashambulio ya kigaidi kushindwa kufaulu.

Polisi wa Uingereza wanaamini watu wanane waliokamatwa ni washukiwa wakuu katika njama ya mashambulio ya mabomu katikati ya mji wa London na shambulio katika uwanja wa ndege wa kimatafia wa Galsgow nchini Scotland. Sita kati yao ni madaktari wakiwemo pia raia mmoja wa Jordan na Muirak.

Wakati huo huo, waziri mkuu wa Uingereza, bwana Gordon Brown ameamuru sheria za kuwaajiri wafanyikazi wa kutoa huduma za afya zinazosimamiwa na serikali, zifanyiwe marekebisho.

Brown amependekeza pia kuundwe baraza la usalama la kitaifa litakalokuwa na kazi ya kutathimini uwezekano wa vitisho vya mashambulio ya kigaidi.