1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON: Virusi vimetoka maabara ya utafiti

5 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBbm

Wizara ya mazingira ya Uingereza imesema,virusi vya ugonjwa wa miguu na midomo vilivyogunduliwa katika ngombe wa shamba moja kusini mwa nchi, vimefanana na vile vinavyofanyiwa utafiti katika kampuni moja ya Kimarekani ilio jirani.

Kwa maoni ya wataalamu,virusi hivyo vimetokea maabara ya kampuni hiyo na kuwaambukiza ngombe katika shamba lililo umbali wa kiasi ya kilomita sita.

Serikali ya Uingereza,imeamaua kwa hiyari kupiga marufuku usafirishaji wa mifugo na bidhaa za wanyama.Hali ya wasiwasi pia imeufanya Umoja wa Ulaya,kupiga marufuku kuagizia mifugo kutoka Uingereza.