1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON : Wachunguzi wa kifo cha Litvinenko kwenda Moscow

4 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCmo

Polisi ya Uingereza imesema itatuma timu ya wapelelezi mjini Moscow wanaochunguza kifo cha Alexander Litvinenko aliekufa kutokana na kutiwa sumu kuzungumza na watu waliokutana na mpelelei huyo wa zamani wa Urusi mjini London muda mfupi kabla ya kifo chake.

Madaktari katika mji mkuu wa Uingereza wanaendelea kuchunguza hali ya Mario Scaramella mtaalamu wa usalama wa Italia ambaye alikutana na Litvinenko siku aliyotiwa sumu. Scaramella alipofanyiwa uchunguzi alionekana kuwa na polonium 210 aina ya sumu ya miale ya nuklea iliomsababishia kifo Litvinenko lakini haounyeshi ishara ya kuathiriwa na sumu hiyo.

Akiwa mahtuti kitandani Litvinenko amemshutumu Rais Vladimir Putin wa Urusi kwa kuamuru kifo chake madai ambayo serikali ya Urusi imeyakanusha.