1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

London. Wakatoliki na Waprotestant watakiwa kugawana madaraka.

14 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD38

Serikali za Uingereza na Ireland zimezindua mapendekezo ya kufufua utawala wa kugawana madaraka kati ya wakatoliki na Waprotestant kwa ajili ya Ireland ya kaskazini.

Waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair na mwenzake wa Ireland ya kaskazini Bertie Ahern, walitangaza hayo baada ya kushindwa kupata muafaka baina ya wanasiasa mahasimu wa Ireland ya kaskazini.

Mazungumzo yalivunjika kuhusiana na kukataa kwa Waprotestant kugawana madaraka na chama cha Wakatoliki cha Sinn Fein pamoja na Wakatoliki kusita kukubali jeshi la polisi la nchi hiyo. Mawaziri wakuu hao wameonya pande zote kukubaliana na mapendekezo hayo katika muda wa mwezi mmoja ama majadiliano juu ya kufikiwa makubaliano ya kugawana madaraka yanaweza kuvunjwa.