1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON: Walibya washinda rufaa yao

28 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC6K

Mahakama ya Uingereza hapo jana iliridhia rufaa ya raia wawili wa Libya kupinga kurudishwa kwao, pamoja na kwamba wamelezwa kuwa ni watu hatari kwa usalama wa Uingereza.

Serikali ya Uingereza imepanga kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo wa mahakama.

Mahakama hiyo maalum ya Rufaa katika masuala ya uhamiaji nchini humo, imesema kuwa walibya hao wawili, ambao wanatambuliwa kwa herufi mbili tu za majina yao, DD na AS, wanakabiliwa na hatari iwapo watarudi kwao.

Kwa mujibu wa mkataba wa haki za binaadamu wa Ulaya ambao Uin gereza imeuridhia, hairuhusiwi kuwarudisha watu katika nchi yao ambako watakabiliwa na hatari ya kimaisha.

Hata hivyo mahakama hiyo imekiri kuwa watu hao wawili ni hatari kwa usalama wa Uingereza, kwani wamekuwa na maingiliano na makundi la Taliban na Al Qaida.

Serikali ya Uingereza imedai kuwa mmoja wa walibya hao DD ni binamu wa Serhane Fakhet ambaye alijilipua wakati wa msako wa polisi wa Uhispania dhidi ya wahusika wa ulipuaji wa mabomu katika treni nchini humo mwaka 2004.