1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON : Wandamana kudai G8 ipige vita umaskini

3 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBvO

Maelfu ya waandamanaji wameandamana katikati ya London kudai viongozi wa Kundi la Mataifa Manane G8 wa nchi zenye maendeleo makubwa ya viwanda duniani watakaokutana mjini Heilligendam nchini Ujerumani wiki ijayo kutimiza ahadi walizotowa huko nyuma za kupiga vita umaskini.

Maandamano hayo yanakuja baada ya miaka miwili ya mkutano wa viongozi wa Kundi la Mataifa Manane G8 uliofanyika huko Gleanagles Scotland nchini Uingereza wakati viongozi hao wa nchi kubwa kabisa duniani walipoahidi kupunguza umaskini kwa nusu ifikapo mwaka 2015.

Waandamanaji walitumia dakika tatu kupiga makelele kwa kutumia vifirimbi,saa za kuamsha na simu za mkononi wakati wakiwa wamejipanga pembezoni mwa mabenki yalioko kwenye Mto Thames na madaraja yalioko pembezoni mwa jengo la bunge.

Inakadiriwa kwamba watu 10,000 wameshiriki maandamano hayo.