1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

London. Watuhumiwa sita wa ugaidi wafikishwa mahakamani.

16 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCaD

Nchini Uingereza , watu sita wamefikishwa mahakamani wakituhumiwa kwa kupanga na kutekeleza mashambulizi ya mabomu ya kujitoa muhanga katika njia za usafiri mjini London.

Mwanzoni mwa kesi hiyo , waendesha mashtaka wamesema watu hao walikuwa wakifanyiakazi katika njama za imani kali za Uislamu, na kulenga mji wa London kiasi cha wiki mbili baada ya mashambulizi ya mabomu ya Julai 7,. 2005, ambapo watu 52 waliuwawa na mamia zaidi kujeruhiwa.

Inaaminika kuwa watuhumiwa hao sita walikuwa wakijaribu kupanga mashambulizi mengine kama hayo.

Hakuna mtu aliyeuwawa ama kujeruhiwa katika mashambulizi hayo kwasababu mabomu hayo yalishindwa kulipuka. Watu hao wamekana madai hayo, wakidai kuwa mabomu hayo yalikuwa ya bandia.