1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON:Bahrain yadai Iran ina uwezo wa kutengeza silaha za nuklia

2 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/C7AW

Mwanamfalme wa Bahrain anadai kuwa Iran inatengeza silaha za nuklia au ina uwezo wa kufanya hilo kwa mujibu wa magazeti ya Uingereza.Hii ni mara ya kwanza kwa taifa la Arabuni kuilaumu Iran waziwazi kwa kutoa maelezo potofu kuhusu mpango wake wa nuklia.Sheikh Salman bin Hamad al –Khalifa aliyefanya mahojiano na waandishi wa habari katika mji mkuu wa Manama aidha anatoa wito wa kupatikana kwa suluhu ya kidiplomasia kati ya mataifa ya magharibi na nchi jirani yake ya Iran kwa mujibu wa gazeti la daily Telegraph.Nchi ya Bahrain ina uongozi wa Kisunni huku asilimia 60 ya wakazi wake wakiwa WaShia.Iran ina Washia wengi.

Iran inakataa katakata kusitisha mpango wake wa nuklia hata baada ya kuwekewa vikwazo na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.Mwishoni mwa mwezi Oktoba Marekani ilitangaza vikwazo vipya dhidi yake na kudai kuwa inafadhili vitendo vya ugaidi.

Vikwazo hivyo vinalenga jeshi la Revolutionary Guard linalolaumiwa kuendeleza ugaidi.Viongozi wa ngazi za juu wa jeshi hilo wanaonya kuwa endapo itahitajika majeshi yao yako tayari kufanya mashambulizi ya kujitoa mhanga katika eneo la Ghuba.Iran kwa upande wake inasisitiza kuwa mpango wake wa nuklia ni wa kutengeza nishati