1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON.Blair ahimiza kupangwe mikakati mipya juu ya mashariki ya kati

15 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCsT

Waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair ameiambia Marekani kwamba njia muafaka katika kuutatua mzozo wa Israel na Plaestina ni kuzihusisha nchi za kiislamu ambazo haziambatani na msimamo mkali kwenye mpango mpya kuhusu Irak.

Blair aliyasema hayo wakati alipofanya mazungumzo na kundi la Marekani lililohusika na kutathmini hali ya nchini Irak linalo wahusisha wanasiasa kutoka vyama vya Republicans na Demokrats.

Kundi hilo litawasilisha tathmini hiyo kwa rais George W Bush wa Marekani katika ikulu ya White House mjini Washington mwezi ujao.

Tathmini hiyo itatoa pia ushauri kuhusu Irak.

Waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair ameitaja Iran kuwa tishio kwa eneo la mashariki ya kati.

Amependekeza mfumo mpya ubuniwe katika mkakati wa kushughulikia maswala ya mashariki ya kati.