1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

London.Blair kumkabidhi madaraka Brown.

11 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC3G

Waziri wa fedha wa Uingereza Gordon Brown anatarajiwa kuanza kipindi cha kampeni ili kuwa waziri mkuu mpya wa nchi hiyo na kiongozi wa chama tawala cha Labour.

Hii inakuja wakati waziri mkuu wa sasa Tony Blair rasmi amemuidhinisha Brown kuwa mrithi wake kama kiongozi wa chama cha Labour.

Blair ametangaza jana Alhamis kuwa atang’atuka madarakani ifikapo Juni 27.

Amewaambia wafuasi wake kuwa licha ya utata mkubwa uliojitokeza kutokana na majeshi ya Uingereza yaliyojihusisha na vita nchini Iraq , lakini alikuwa kila mara akifanya kile alichohisi kuwa ni sahihi kwa nchi yake.

Wakati huo huo waziri huyo mkuu anatarajiwa kukutana na rais anayeondoka madarakani nchini Ufaransa Jacques Chirac na rais mteule Nicolas sarkozy mjini Paris.