1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

London.Iran bado ina nafasi ya mazungumzo.

7 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD5H

Mataifa sita yenye nguvu duniani yamekubaliana kujadili uwezekano wa vikwazo vitakavyoiadhibu Iran kwa kushindwa kusitisha mpango wake wa kinuklia lakini wamesema kuwa bado wanaweka mlango wazi juu ya majadiliano na Iran.

Iran ilishindwa kutimiza muda wa mwisho wa August 31 uliowekwa na baraza la usalama la umoja wa mataifa kuweza kusitisha urutubishaji wa madini ya urani.

Mataifa ya magharibi yanashaka kuwa mpango huo wa Iran ni kisingizio cha kutengeneza bomu la atomic.

Iran inasema kuwa mpango wake ni kwa ajili ya matumizi ya amani.

Baada ya mazungumzo na mawaziri kutoka Marekani, Ufaransa, ujerumani, Russia, na China , waziri wa mambo ya kigeni wa Uingereza Margaret Beckett amesema kuwa mawaziri hao wasikitishwa sana na taarifa ya mkuu wa sera za mambo ya kigeni wa umoja wa Ulaya Javier Solana kuwa mazungumzo yake yaliyofanyika kwa muda wa miezi minne , yameshindwa kuishawishi Iran.

Marekani ikiungwa mkono na Uingereza , inashinikiza kwa nguvu nchi hiyo kuwekewa vikwazo, lakini Russia na China zinapinga wazo hilo.