1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON:Maandamano ya kumwuunga mkono Aung San Suu Kyi leo

24 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7DC

Maandamano ya kupinga kuendelea kuwekwa mahabusu kiongozi wa upinzani Aung San Suu Kyi nchini Mynmar yatafanyika katika miji kadhaa ikiwa pamoja na London, Berlin, Paris, Washington na Cape Town leo unapotimu mwaka wa 12 tokea mwanasiasa huyo awekwe mahabusu ya nyumbani.

Watu katika miji hiyo wataandamana mbele ya ofisi za ubalozi wa China.

China inahesabika miongoni mwa nchi zenye uzito mkubwa juu ya utawala wa kijeshi nchini Mynmar.