1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON:majeshi ya mfungamano yanakaribia kuukimbia mji wa Basra?

19 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBXu

Mshauri wa kijeshi wa Marekani amesema huenda majeshi ya Uingereza yakaondoka mji wa Basra,kusini mwa Irak katika namna ya kuumbuka.

Mshauri huyo bwana Stephen Biddle ambae ni mjumbe wa baraza la Marekani linaloshughulikia uhusiano wa nchi za nje ameliambia gazeti la Sunday Times la Uingereza kwamba majeshi ya mfungamano hayana tena uwezo wa kuudhibiti mji huo.

Ameeleza kuwa wapinzani ndiyo wenye usemi katika mji wa Basra na pana uwezekano wa majeshi ya mfungamano kutimuliwa kutoka kwenye mji huo.