1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON:Somalia yapoteza fursa ya kupata amani na ustawi

24 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCYI

Naibu mwenyekiti wa Umoja wa Afrika AU,Patrick Mazimhaka anasema kuwa nafasi ya kupata ustawi na amani nchini Somalia inapotea.Kiongozi huyo aliyasema hayo alipozungumza na gazeti la Financial Times hii leo.Aidha aliongeza kuwa mpaka sasa bado hakuna taifa lolote lisilo la bara la Afrika lililokubali kugharamia kikosi cha majeshi alfu 8 ya kulinda amani yanayopangwa kuepelekwa nchini Somalia.

Bwana Mazimhaka alisisitiza umuhimu wa kupeleka majeshi hayo ya kulinda amani haraka iwezekanavyo.Baraza la Usalama la Umoja wa Afrika AU limeshaidhinisha hatua ya kupelekwa majeshi alfu 8 ya kulibda amani katika mpango wa Ujumbe maalum wa Somalia AMISOM baada ya mkutano mjini Addis Ababa,Ethiopia wiki iliyopita.

Kulingana na taarifa ya Umoja huo zaidi ya majeshi alfu 2500 ambayo ni thuluthi moja ya kikosi kilichopangwa kupelekwa yatapelekwa Somalia haraka iwezekanavyo katika kipindi cha miezi sita y kwanza.

Kikosi hicho cha majeshi alfu 8 baadaye kinaratajiwa kuchukua majukumu kama ya Umoja wa Mataifa ili kufikia malengo ya kukarabati serikali ya Muda ya Somalia iliyoungwa mkono na majeshi ya Ethiopia mwezi jana ili kufurusha wapiganaji wa mahakama za kiislamu.

Hata hivyo ni mataifa mawili pekee yaliyokubali kupeleka majeshi yao Somalia mpaka sasa.Wakati huohuo majeshi ya Ethiopia yalianza kuondoka nchini humo haopo jana jambo linalosababisha raia wa Somalia kuhofia usalama wao.