1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

London.Tamasha la muziki kupambana na uharibifu wa mazingira lafana.

8 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBku

Mwanamuziki mashuhuri Madonna aliongoza wito unaotolewa na wanamuziki duniani kote katika mapambano dhidi ya utojo duniani.

Pekee mjini London katika uwanja wa Wembley, kiasi cha mashabiki wa muziki wapatao 60,000 walihudhuria katika kuunga mkono tamasha la siku nzima la muziki linalojulikana kama Live Earth , lililotayarishwa na makamu wa rais wa zamani wa Marekani ambayo ni mwanaharakati wa ulinzi wa mazingira Al Gore.

Matamasha yaliyosheheni wanamuziki nyota mjini New York na Rio de Janeiro yalikamilisha tukio hilo lililofanyika kwa muda wa saa 24 ambapo watayarishaji waliwataka washiriki kupunguza utoaji wao wa gesi zinazoharibu mazingira na kuzitaka serikali na viwanda kufanya hivyo pia.

Mamia kwa maelfu ya watu walihudhuria pia maonyesho kama hayo mjini Sydney, Tokyo, Shanghai, Johannesburg, Hamburg na Washington. Mapato kutokana na maonyesho hayo ya muziki yatakwenda katika taasisi ya Gore inayopambana katika ulinzi wa mazingira.