1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON.Uhusiano wa Uingereza na Urusi wazorota

27 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCp6

Waziri mmoja wa Uingereza amekiri kwamba uhusian o kati ya nchi yake na Urusi umezorota kufuatia kifo cha kachero wa zamani wa Urusi Alexndaer Litvinenko mjini London.

Wachunguzi wa mauaji hayo kutoka Uingereza wanatarajiwa kwenda mjini Moskow, Urusi na Roma, Italia kuendeleza uchunguzi wao.

Madaktari wamethibitisha kwamba kachero huyo wa zamani aliuwawa kwa sumu hatari ya polonium 210 iliyo onekana katika mikojo ya kachero huyo.

Chembe chembe za sumu hiyo pia zimegunduliwa katika baa ya Sushi na hoteli aliyokutana na watu ambao baadae akaanza kuugua.

Litvinenko aliyemkosoa rais Vladmir Puttin wa Urusi alikuwa anachunguza kifo cha mwandishi habari Anna Politkosvskaya.