1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON:Uingereza yakumbwa na ugonjwa wa miguu na midomo kwa wanyama

4 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBc8

Uingereza imepiga marufuku usafirishaji wa ng´ombe, kondoo na nguruwe kufuatia kuibuka kwa ugonjwa wa miguu na midomo katika shamba moja huko kusini mwa nchi hiyo.

Waziri Mkuu wa Uingereza Gordon Brown alisimamia kikao cha kamati ya dharura ya serikali iitwayo COBRA kuzungumzia juu ya suala hilo.

OTON: GORDON

Brown anasema kuwa kwa upande wa serikali watafanya kila wawezalo haraka sana ili kupata ushahidi wa kisayansi kujua chanzo cha maradhi hayo.

Maradhi hayo ya miguu na midogo kwa wanyama yalilipuka mwaka 2001 na kupelekea mamilioni ya wanyama kuchinjwa kote nchini.