1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON:Viongozi wa Uingereza na Marekani waahidi kushirikiana

31 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBdS

Waziri Mkuu wa Uingereza Gordon Brown amefanya mkutano wake wa kwanza na Rais George Bush wa Marekani tangu kuchukua wadhifa huo mwezi jana.Ziara ya Bwana Brown inafanyika kukiwa na tetesi kwamba uhusiano kati ya nchi hizo mbili Marekani na Uingereza huenda ukawa rasmi baada ya mtangulizi wa Bwana Brown ,Tony Blair kuondoka.Katika mazungumzo hayo ya Camp David viongozi hao wawili walithibitisha kuimarisha uhusiano kati yao.

''Tunaunga mkono uhusiano kati yetu kwani tuna mtazamo sawa.Tuna amini kuwa ni muhimu kuwa na uhuru na haki.''

Bwana Brown anasisitiza umuhimu wa ushirikiano wao.

''Nadhani tunakubali kuwa changamoto zote zitakabiliwa pale Uingereza na Marekani wanashirikiana kwa njia ambayo itaimarika katika miaka ijayo''

Waziri Mkuu Gordon Brown alisema kuwa wanaafikiana kuhusu suala la Iran

''Kuhusu suala la Iran tunakubaliana kuwa vikwazo vilivyowekwa vinafanya kazi na hatua inayofuatia ni kuviongeza makali kama azimio la Umoja wa mataifa linavyosema.''

Bwana Brown anatarajiwa kuelekea mjini Newyork ili kukutana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon na kuhutubia baraza la Umoja wa Mataifa.