1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON:Wanamaji wa Uingereza waliokamatwa wako salama,yasema Iran

28 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCEp

Nchi ya Iran inashikilia kuwa wanamaji 15 wa Uingereza waliowakamata wiki jana wako salama ingawaje bado inakataa kueleza waliko aidha kutowaruhusu mabalozi wa Uingereza kuwatembelea.Waziri Mkuu wa Uingereza Tony Blair anaionya Iran kuwaachia raia wake hao haraka iwezekanavyo na kudai kuwa waliingia katika eneo hilo kikazi.

Uingereza kwa upande wake inajiandaa kutoa ushahidi kuwa wanamaji hao walikamatwa kimakosa.Kulingana na BBC Uingereza iko tayari kubadili mbinu zake za kidiplomasia baada ya Waziri Mkuu Tony Blair kuonya kuwa majadiliano hayo huenda yakafuata mkondo mpya endapo suluhu haipatikani.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Uingereza Margaret Beckett alikatiza ziara yake ya Uturuki baada ya mazungumzo yake na mwenzake wa Iran Manoucher Mottaki kuambulia patupu.

Iran kwa upande wake inashikilia kuwa wanamaji hao waliingia katika eneo lao bila ruhusa jambo ambalo Iraq inapinga.