1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON:Watoto bado wanatembea na silaha nchini Jamhuri ya kidemkrasi ya Kongo

12 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD3f

Shirika linalotetea haki za binadamu duniani Amnesty International limesema kwamba maalfu ya watoto nchini Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo bado wanadhibitiwa na makundi ya waasi wenye silaha.

Shirika hilo limeeleza kuwa hata baada ya miaka mitatu tokea kumalizika vita nchini humo watoto wapatao alfu 11 bado wana silaha mikononi.

Watu wapatao milioni nne waliuawa katika vita vya miaka mitano nchini Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo ambapo watoto pia walitumika kama askari.

Watoto zaidi alfu 30 walihusishwa katika vita hiyvo.