1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LOS ANGELES: Rais wa zamani wa Marekani, Gerald Ford afariki dunia.

27 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCfs

Rais wa Zamani wa Marekani, Gerald Ford, amefariki dunia. Taarifa ya kifo cha Gerald Ford aliyefariki California akiwa na umri wa miaka 93, ilitolewa na mkewe.

Gerald Ford ndiye rais wa pekee wa Marekani ambaye hakuchaguliwa na umma.

Aliteuliwa kuwa makamu wa rais na mwaka 1973 akachukua madaraka kumrithi Richard Nixon aliyelazimika kuondoka madarakani kutokana na kashfa ya Watergate.

Gerald Ford amekuwa akikabiliwa na homa ya kichomi tangu Januari mwaka huu na amewahi kufanyiwa upasuaji wa moyo mara mbili