1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Luiz Gustavo ajiunga na Wolfsburg

16 Agosti 2013

Vfl Wolfsburg wamefanikiwa kuinyakua saini ya mchezaji wa Bayern Munich Luiz Gustavo. Gustavo amesaini mkataba wa miaka minne na Wolfsburg na tayari amezinduliwa rasmi katika klabu hiyo

https://p.dw.com/p/19RED
GettyImages 153030641 Bayern Munich's Brazilian midfielder Luiz Gustavo celebrates his goal (0-1) during the German first division Bundesliga football match SV Werder Bremen vs FC Bayern Munich in Bremen, northern Germany, on September 29, 2012. AFP PHOTO / JOHANNES EISELE DFL RULES TO LIMIT THE ONLINE USAGE DURING MATCH TIME TO 15 PICTURES PER MATCH. IMAGE SEQUENCES TO SIMULATE VIDEO IS NOT ALLOWED AT ANY TIME. FOR FURTHER QUERIES PLEASE CONTACT DFL DIRECTLY AT + 49 69 650050. (Photo credit should read JOHANNES EISELE/AFP/GettyImages)
FC Bayern München - Werder BremenPicha: Getty Images

Mkataba huo unaaminika kuwa kati ya euro milioni 15 na 20. Gustavo raia wa Brazil mwenye umri wa miaka 26 alikuwa amehusishwa na uhamisho wa kujiunga na Arsenal. Alijiunga na Bayern akitokea Hoffenheim mnamo Januari 2011, na amaeomba kuihama klabu hiyo ili kupata nafasi ya kucheza katika timu ya kwanza kwa sababu nafasi zake za kucheza kila mara katika klabu ya Bayern zilikuwa chache msimu uliopita.

Kwingeneko Werder Bremen wamesaini mshambuliaji wa Argentina Franco Di Santom kutoka klabu ya England Wigan.

Ilkay Gundogan anatarajiwa kuwa nje mkekani kwa wiki mbili
Ilkay Gundogan anatarajiwa kuwa nje mkekani kwa wiki mbiliPicha: AFP/Getty Images

Di Santo mwenye umri wa miaka 24 amejiunga na mshambuliaji wa zamani wa Bayern Nils Petersen baada ya mkataba wake na Wigan kukamilika mwishoni mwa msimu uliopita.

Katika habari yingine za Bundesliga ni kuwa kiungo wa Borussia Dortmund Ilkay Gundogan atakuwa mkekani kwa karibu wiki mbili baada ya kupata jeraha la mgongo wakati akiichezea timu ya taifa ya Ujerumani katikati ya wiki.

Gundogan ambaye alifunga goli la kwanza la Ujerumani katika mchuano wao dhidi ya Paraguay uliokamilika kwa sare ya kufungana mabao matatu kwa matatu, aliondolewa uwanjani katika dakika ya 26 wakati alipoanza kuhisi maumivu. Hii ina maana kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 atakosa mchuano wa nyumbani wa Dortmund dhidiy a Eintracht Braunschweig hapo kesho Jumapili na pia dhidi ya Werder Bremen mnamo Agosti 3.

Kocha wa Borussia Dortmund Jurgen Klopp huenda akawajumuisha kikosini wachezaji wa viungo Sven Bender na Nuri Sahin wakati pia mchezaji mpya Henrikh Mkhitaryan akitarajiwa kucheza baada ya kupona jeraha la kifundo cha mguu.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/reuters

Mhariri: Yusuf Saumu