1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LUSAKA : Chiluba atakiwa aikabidhi serikali nyumba yake

12 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBsd

Rais wa zamani wa Zambia Fredrick Chiluba lazima asalimishe nyumba yake kwa serikali kama nusu ya malipo ya dola milioni 58 alizoamuriwa kulipa katika kesi ya rushwa.

Hakimu wa Uingereza Peter Smith aliamuru kutwaliwa kwa mali yake hapo Jumatatu wakati wa kusikiliza kesi juu ya namna Chiluba anavyotakiwa kulipa fedha hizo baada ya mahkama ya Uingereza kuhukumu kuwa aliziiba wakati akiwa madarakani hapo mwaka 1991 hadi mwaka 2001.

Mwanasheria Mkuu Mumba Malila amesema mahkama imemuamuru rais huyo wa zamani akabidhi umiliki wa nyumba yake pamoja na mali nyengine zinazohamishika zilizonunuliwa hapo tarehe 14 mwezi wa Desemba mwaka 2001 za thamani ya dola 297,580.