1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LUSAKA : Chiluba yu mgonjwa mno kusimama kizimbani

18 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCrb
Kitambulisho cha amani ya Mashariki ya kati
Kitambulisho cha amani ya Mashariki ya kati

Mahkama ya Zambia imehukumu kwamba rais wa zamani wa nchi hiyo Frederick Chiluba ambaye hivi sasa anashtakiwa kwa rushwa yu mgonjwa sana kuweza kufika mahkamani na lazima aruhusiwe kusafiri nchi za nje kwa matibabu.

Chiluba anashtakiwa kwa kuiba fedha za umma dola milioni 488 wakati akiwa rais lakini kesi yake ya miaka miwili imekuwa ikitibuliwa na matatizo ya moyo na figo ambayo yamekuwa yakimsumbuwa tokea mwaka jana.Tayari mwaka huu ametumia miezi sita akiwa hospitalini Afrika Kusini.

Mahkama hiyo ya mfawidhi imetowa hukumu yake hiyo hapo jana jioni.