1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LUSAKA : Mikutano ya kisiasa marufuku

15 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCj7

Serikali ya Zambia imepiga marufuku maandamano ya kisiasa na kuiweka nchi hiyo kwenye hali kubwa ya tahadhari kukabliana na vitisho vya kiongozi wa upinzani Michael Sata.

Naibu Waziri wa mambo ya ndani Chrispine Musosha ameuambia mkutano wa waandishi wa habari kwa Sata ambaye alishindwa chupu chupu katika uchaguzi wa Urais hapo mwezi wa Septemba na Rais Levy Mwanawaswa amekuwa akihujumu hali ya usalama nchini Zambia kwa kile serikali inachokielezea kuwa hotuba zake za uchochezi katika maandamano ya hadhara siku za hivi karibuni.

Musosha amesema polisi haitowa tena vibali vya mikutano ya kisiasa hadi hapo yatakapotolewa maelezo zaidi na kwamba hawatowaruhusu tena watu kuvuruga amani na usalama nchini humo.