1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LUSAKA: Rais wa Zambia Levy Mwanawasa ajiandaa kutawazwa kwa mhula wa pili

3 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD6Z

Rais wa Zambia Levy Mwanawasa ambae alitangazwa jana mshindi katika uchaguzi uliyofanyika wiki iliyopita. Kiongozi wa korti kuu Ernest Sakala, alisema kuwa Levy Patrick Mwanawasa, aliibuka mshindi na kura 1,177,846 dhidi ya Michael Sata aliyeambulia kura 804,748. Kwa sasa Levy Mwanawasa anajiandaa kuanza mhula wa pili wa miaka mingine mitano Alhamisi wiki hii akiahidi kuimarisha mpango wake wa kiuchumi kwa kuendeleza uhusiano bora na nchi fadhili za magharibi ambazo ziliwekeza mitaji mikubwa ya kiasi cha bilioni 1 na milioni 400 za dolla za kimarekani katika madini ya shaba na kobalti.

Mpinzani wake Michael Sata alitoa wito wa utulivu hapo jana kufuatia siku nzima ya ghasia zilizozushwa na wafuasi wake wakidai kuwa kulitokea wizi wa kura kumpa ushindi Levy Mwanawasa. Michael Sata kiongozi wa chama cha Patriotic Front, alikuwa akiongoza kwa kura katika matokeo ya mwanzo ya uchaguzi.