1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Luxembourg.Mgogoro wa Uturuki na Cyprus bado haujapatiwa suluhisho.

17 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD20

Umoja wa Ulaya na Uturuki, zimeshindwa kusuluhisha mgogoro unaohusika na Uturuki kukaa kusawazisha uhusiano wake na Cyprus, jambo ambalo linazidi kuhatarisha na fasi ya nchi hiyo yenye waislamu wengi, kuingia katika Umoja wa Ulayawenye wanachama 25.

Baada ya mawaziri wa kigeni wa Umoja huo kukutana na waziri mwenziwe wa Uturuki Abdallah gul mjini Luxembourg, waziri wa Ujerumani, Frank-Walter Steinmeier aliwaambia waandishi wa habari kuwa, Gul hakutoa ahadi yoyote ile ya kuruhusu meli za Cyprus kutumia bandari za Uturuki.

Hilo ni sharti kuu la Umoja wa Ulaya linalohitaji kutimizwa na Uturuki ili kuweza kupokewa katika Umoja huo.

Waziri Steinmeier akaongezea kwa kusema.

“Ni matumaini yangu kuwa katika kipindi cha wiki zijazo, mafanikio yatapatikana, kwani ni lazima kuwa na maendeleo au utaratibu wa kujiunga na Umoja huo utavurugika vibaya“.

Wakati huo huo waziri Steinmeier akaongezea kuwa, anaunga mkono pendekezo jipya lililotolewa na Finland, kuiruhusu biashara huru kati ya Umoja wa Ulaya na bandari ya Famagusta iliyo katika eneo la Kituruki kaskazini mwa Cyprus.

Uturuki kwa upande wake inatakiwa iziruhusu meli za Cyprus kutumia baadhi ya bandari za Uturuki.