1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

M23, FDLR wawekewa vikwazo

1 Januari 2013

Baraza a Usalama la Umoja wa Mataifa limewawekea vikwazo waasi wa M23 katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo pamoja na kundi lingine washirika wao la FDLR kutoka Rwanda.

https://p.dw.com/p/17Bn3
Abdul-Ilah al-Khatib, left, United Nations Special Envoy to Libya, briefs members of the Security Council on the situation in Libya at U.N. Headquarters, Monday, April 4, 2011. (AP Photo/David Karp)
UN-Sicherheitsrat 2011Picha: AP

Viongozi wa makundi hayo wamewekewa vikwazo hivyo kutokana na kuzusha machafuko katika eneo la mashariki ya Kongo. Viongozi hao Jean-Marie Runiga Lugerero na Luteni Kanali Eric Badege wanaoshutumiwa kwa mauwaji ya wanawake na watoto.

Kamati ya baraza hilo ambayo ndiyo yenye jukumu la kusimamia utekelezaji wa vikwazo hivyo nchini Kongo imewazuia kusafiri pamoja na kuzuia mali za viongozi hao.

Balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa Suzan Rice, amesema kuwa wanamatumaini uamuzi huo utasaidia katika harakati za kurejesha amani kwenye Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. "Tunawataka vingozi wote wa ngazi za juu wa M23 na FDLR kujitoa kwenye makundi hayo ili kujiepusha na vikwazo hivyo.

Susan Rice, Balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa
Susan Rice, Balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa

Hapo kabla baraza hilo liliweka vikwazo kwa viongozi wa kundi la M23 katika mwezi wa Novemba mwaka uliopita ambao ni Sultani Makenga, Baudoin Ngaruye na Innocent Kaina lakini sasa limeweka vikwazo kwa makundi yote mawili.

Shutuma za ukiukaji wa haki za binaadamu

Afisi ya Kamishna wa Haki za Binaadamu wa Umoja wa Mataifa imewatuhumu waasi wa M23 kwa kuhusikana mauwaji ya kinyama, kuwalazimisha watu kukimbia makaazi yao, vitendo vya ubakaji na masuala mengijne ya ukiukaji wa haki za binaadamu kwa raia wa ndani na nje ya mji wa Goma mashariki mwa Kongo katika kipindi cha mwezi Novemba. Hata hivyo M23 wamekanusha tuhuma hizo.

"Kwa miaka kadhaa sasa kundi la FDLR limekuwa likifanya vitendo vya kinyama dhidi ya raia na limeendelea kubakia kitisho kwa amani ya kwenye majimbo ya Kivu ya Kaskazini na Kusini", alisema Rice.

Aliendelea kusema kuwa uamuzi wa sasa wa vikwazo dhidi ya FDLR ni hatua muhimu kukomesha visa vya kundi hilo na kuelekea hali ya amani na usalama kwenye eneo hilo.

Kiongozi wa M-23 Jean-Marie Runiga
Kiongozi wa M-23 Jean-Marie RunigaPicha: AP

Rwanda kuchukua nafasi barazani humo leo

Uamuzi huo wa vikwazo umefanyika ikiwa ni saa chache kabla ya Rwanda kuchukua nafasi yake kwenye baraza hilo hii leo (1.1.2013) kama mwanachama asiye wa kudumu.

Umoja wa Mataifa unazituhumu nchi za Rwanda na Uganda kuwa zinawaunga mkono waasi wa M23 katika eneo la mashariki ya Congo.

Rais Paul Kagame wa Rwanda
Rais Paul Kagame wa RwandaPicha: picture-alliance/dpa

Ingawa Baraza la Usalama limekuwa likisema mara kadhaa kuwa kuna mataifa ya nje yanawaunga mkno waasi, lakini halijawahi kuitaja Rwanda au Uganda kwa jina hadi sasa.

Rice ameonya kuwa kuna uwezekano wa kuchukuliwa hatua zaidi pale itakapohitajika, kwa mataifa yoyote yatakayoendelea na harakati zao za kuwaunga mkono waasi kutokea nje au kuwasaidia waasi hao kukwepa vikwazo vilivyowekwa.

Ingawa Baraza la Usalama limekuwa likisema mara kadhaa kuwa kuna mataifa ya nje yanawaunga mkono waasi, lakini halijawahi kuitaja Rwanda au Uganda kwa jina hadi sasa.

Mwandishi: Stumai George/Afpe

Mhariri: Sekione Kitojo