1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maabara ya mimea asilia

Jeppesen, Helle 26 Februari 2008

Maabara ya kuhifadhi mimea ya kale isitoweke imefunguliwa leo katika ncha ya kaskazini ya dunia yetu

https://p.dw.com/p/DDN9
Maabara ya minmea asiliaPicha: Mari Tefre/Global Crop Diversity Trust

Naiwe kwasababu ya mabadiliko ya hali ya hewa,hataza ,faida za kiuchumi,au maradhi,mimea mingi ya jadi inakabiliwa na hatari ya kutoweka.Aina nyingi za mimea imetoweka moja kwa moja kwasababu mapato yake ni haba ikilinganishwa na mimea mipya.Na ikifika siku ambapo mimea hiyo asilia itahitajika kwasababu ya umuhimu wake kwa tiba,haitakutikana kokote.Labda katika maktaba ya mimea ambako mbegu za mimea zinatunzwa na kuhifadhiwa.Nchi nyingi zimeshaamua kufanya hivyo kwa daraja ya kitaifa-lakini mimea jumla asilia ya dunia yetu hii imewekwa na kutunzwa Spitzbergen,umbali wa kilomita 800 ya ncha ya kaskazini ya dunia.Maabara ya mimea katika eneo hilo la baridi kali imezinduliwa hii leo.
"Ni maktaba ya kweli ya maisha hii,ni historia ya maisha yetu katika sayari hii,tangu enzi za jamii ya wawindaji na mkusanyiko wa watu.Mimea hii,aaina hizi tofauti za mimea zinatusimulia historia halisi ya kilimo na zinatueleza pia juu ya historia ya utamaduni wa binaadam."
Cary Fowler amekua akijishulisha na taaluma ya viini vya urithi wa mimea tangu miaka 30 iliyopita.Mkurugenzi huyo wa shirika la Global Crop Diversity Trust ameshawahi kutunikiwa zawadi mbadala ya amani ya Nobel mwaka 1985 kwa shughuli zake za kuhifadhi aina mbali mbali za mimea asilia. Katika kipindi chote hicho cha shughuli zake ameweza kujionea jinsi nchi zaidi zinavyowajibika kufungua maabara ili kuhifadhi mimea asilia isitoweke.
Hekalu maalum limezinduliwa hii leo huko Spitzbergen ,katika ncha ya kaskazini ya dunia yetu kuhifadhi mimea na mbegu zote asilia.Ni hekalu lililojengwa ndani ya mlima. Wataalam wanaamini litaendelea kuwepo kwa miaka elfu ijayo bila ya mabadiliko yoyote.
"Maabara ya mimea ni mahala ambako mbengu za mimea zinahifadhiwa katika mahala baridi na kila ya baada ya miaka 20 hivi mimea hiyo na mbegu zinabidi zioteshwe upya shambani au katika bustani maalum zinazozingatia hali ya hewa,ili iweze kuzaliana kwakua mbegu haziwezi kuhifadhiwa milele."
Professor Andreas Graner anaongoza taasisi ya Leibnitz ya viini vya uridhi wa mimea na uchunguzi wa mimea asilia huko Gatersleben.Yeye pia ni mkurugenzi wa maabara ya kuhifadhi mimea nchini Ujerumani.
Ndani ya maabara hiyo kuna nafasi ya kutosha kuweza kuhiufadhiwa sampuli zisizopungua milioni nne na nusu za mimea.Hadi sasa mimea milioni moja na nusu imekusanywa ndani ya hekalu hiyo.Mimea hiyo inaanzia nafaka,na mazao mengine yanayoweza kusaidia kupambana na njaa katika nchi za ulimwengu wa tatu,aina za matunda yanayoanza kutoweka kwasababu hayaleti tija inayotakikana kiuchumi na kadhalika.
Shughuli za maabara hiyo zinagharimiwa na wakfu wa Bill na Melinda Gate,Umoja wa mataifa,serikali ya norway na baadhi ya nchi ikiwemo pia Ujerumani.