1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maafa ya mafuriko nchini Pakistan.

Abdu Said Mtullya16 Agosti 2010

Katibu Mkuu wa Mataifa Ban Ki-Moon atoa mwito wa kuharakisha misaada ya fedha kwa ajili ya Pakistan

https://p.dw.com/p/OoOj
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon akiwafariji watu wa Pakistan.Picha: AP

ISLAMABAD:
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameitaka jumuiya ya kimataifa iharakishe misaada ya fedha kwa ajili ya watu walioathirika na maafa ya mafuriko nchini Pakistan.

Kwa mujibu wa taarifa ya Umoja wa Mataifa mpaka sasa ni robo tu ya msaada wa dola milioni 460 zilizohitajika kwanza uliopelekwa nchini humo. Katibu Mkuu Ban Ki moon alishtushwa na kiwango cha maangamizi na shida zinazowasibu watu,baada ya kuziona sehemu zilizokumbwa na maafa hayo ,kutokea kwenye ndege.

Ban Ki moon pia alikutana na rais Asif Ali Zardari na waziri mkuu wa Yusuf Raza Gilani.

Mafuriko bado yanaendelea katika kiwango kilekile kwa wiki ya pili sasa, kaskazini magharibi mwa Pakistan na katika majimbo ya Sindh na Punjab.Watu zaidi ya1600 wameshakufa kutokana na mafuriko hayo na Umoja wa Mataifa umesema watu milioni sita sasa wanategemea misaada ili kukidhi mahitaji yao ya maisha.Na kwa mujibu wa taarifa ya serikali ya Pakistan watu milioni 20 wameathirika na mafuriko yaliyoikumba nchi hiyo.

Ujerumani imeongeza fedha kwa ajili ya msaada wa dharura kwa Pakistan hadi kufikia Euro milioni 15.