1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maafikiano kuhusu Mpango wa kufufua Uchumi Marekani

P.Martin7 Februari 2009

Wajumbe wa vyama vya Demokratik na Republikan katika Baraza la Seneti nchini Marekani wamekubaliana na pendekezo la muafaka wa mpango wa kusaidia uchumi nchini humo.

https://p.dw.com/p/Gp4r
U.S. President Barack Obama (R) and Treasury Secretary Timothy Geithner announce new rules regarding executive pay for bailout recipients, at the White House on 04 February 2009. The administration has imposed a cap of $500,000 on the compensation of executives at companies that receive large amounts of taxpayer funded bailout money. EPA/MATTHEW CAVANAUGH +++(c) dpa - Report+++
Rais wa Marekani Barack Obama(kulia) na Waziri wa Fedha Timothy Geithner.Picha: picture-alliance/ dpa

Mpango huo wa muafaka ulio na thamani ya dola bilioni 780 ulikubaliwa baada ya kufanywa majadiliano magumu kati ya pande hizo mbili.Wajumbe wa Seneti walikubali kuupunguza mpango wa awali kwa kiasi cha dola bilioni 150.

Rais wa Marekani Barack Obama amewahimiza wabunge kutochelewa zaidi kuidhinisha mpango huo wa maafikiano.Ameonya, kuwa uchumi wa nchi utakumbwa na maafa ikiwa hautopitishwa haraka bungeni. Hapo awali tarakimu zilizotangazwa zilionyesha kuwa kiasi ya watu 600,000 walipoteza kazi katika mwezi wa Januari.Sasa ukosefu wa ajira umefikia asilimia 7.6 hicho kikiwa kiwango cha juu kabisa tangu mwaka 1992.